Resource Monday, August 11 2025 08:47 GMT

Uelewa kuhusu sheria za vitendo vya kashfa Tanzania

Sheria za kashfa zikitumika kwa usahihi, zinatarajiwa kulinda watu binafsi na watu maalumu dhidi ya taarifa za uongo zinazoweza kuharibu sifa yao. Ingawaje, sheria za madai na za jinai za kashfa zikitumika vibaya zinaweza kuzuia mijadala ya wazi ya umma.

Mwongozo huu unalenga kuwapatia waandishi wa habari uelewa kwa vitendo kuhusu sheria za kashfa/kuharibu sifa ya mtu pamoja na hatua wanazoweza kuchukua ili kupunguza uwezekano wa kuwajibika kisheria kulingana na sheria hizo nchini Tanzania. Uelewa huu utawawezesha waandishi wa habari kufahamu haki na wajibu wao wa kisheria na kuwawezesha kuendelea kutoa taarifa za masuala yenye umuhimu kwa masilahi ya umma. Mwongozo huu unajumuisha mawanda ya sheria za kashfa, mwenendo wa mashauri ya jinai na madai mahakamani, utetezi dhidi ya madai ya kashfa, adhabu zinazotolewa dhidi ya kashfa na hatua za tahadhari zinazoweza kuchukuliwa ili kupunguza hatari ya kuwajibika kisheria. Mwongozo huu umeandaliwa na Thomson Reuters Foundation pamoja na iWatch Africa, kutumia utafiti wa kisheria wa bila malipo (pro bono) uliotolewa na Ideal Law Group.

Download PDF

Download pdf: Download PDF